21 Septemba 2025 - 19:25
Yemen katika Macho na Moyo wa Sayyid Hassan Nasrallah katika Miaka 11 ya Mapinduzi ya Yemen

Watu wa Yemen katika kumbukumbu ya miaka 11 ya ushindi wa Mapinduzi yao wanapanga kufanya maadhimisho ya kumbukumbu ya Sayyid wa Muqawama, kwa kuwa uhusiano wa Sayyid Muqawama na wananchi pamoja na viongozi wa Yemen ulikuwa ni uhusiano wa pande mbili uliojaa mapenzi na heshima.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Mapinduzi ya Septemba 21, 2014 hayakuwa tukio la kupita katika historia ya Yemen, bali yalikuwa ni mwitikio wa asili dhidi ya utawala wa Mansur Hadi uliogeuza Yemen kuwa uwanja wa kuingiliwa na wageni na kunyima wananchi wake uhuru wa kufanya maamuzi ya kisiasa.

Yemen katika Macho na Moyo wa Sayyid Hassan Nasrallah katika Miaka 11 ya Mapinduzi ya Yemen

Leo hii, wananchi wa Yemen katika kumbukumbu ya miaka 11 ya ushindi wa Mapinduzi yao, wakiwa chini ya mzingiro dhalimu na vita kamili na utawala wa Kizayuni, wanasisitiza kuendelea na muqawama wao.

Sehemu kubwa ya maisha ya Mapinduzi ya Yemen imepita katika vita vya kulazimishwa na jukumu la kuunga mkono watu wa Palestina huko Gaza. Miaka 8 ya uvamizi wa muungano wa Saudi na Marekani dhidi ya Yemen na karibu miaka 2 ya kusimama imara kuwatetea watu wa Gaza na kusimamia mlango muhimu zaidi wa bahari ya Kimataifa katika Bahari Nyekundu, vimewapa wananchi wa Yemen heshima na utukufu.

Kama alivyosema kiongozi wa Mapinduzi ya Yemen, Sayyid Abdulmalik al-Houthi mwaka uliopita:

“Mapinduzi ya Septemba 21 ni mafanikio halisi kwa wananchi wa Yemen. Hatua zote zilizochukuliwa katika mchakato wa Mapinduzi haya zilikuwa za Kiyemeni kwa asili, bila ushawishi wa kigeni. Mapinduzi haya yatakuwa na matunda makubwa na kuyajibu matarajio ya wananchi wa Yemen. Kwa miaka 11, licha ya changamoto nyingi, wananchi wa Yemen wameendelea kulinda mafanikio ya Mapinduzi na kuyapanua zaidi. Upande unaopinga Mapinduzi haya, wakiongozwa na Wamarekani na utawala wa Kizayuni, ndio walioshindwa zaidi, kwa kuwa wamepoteza udhibiti wao wa moja kwa moja dhidi ya Yemen.”

Katika siku hizi za kumbukumbu ya Sayyid mashahidi wa muqawama, shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, na kumbukumbu ya miaka 11 ya ushindi wa Mapinduzi ya Yemen, tunapaswa kuuangalia Yemen kwa macho ya Sayyid wa Muqawama. Yeye kila mara katika miaka ya uvamizi wa muungano wa Marekani na Saudi alisisitiza kusimama pamoja na wananchi na viongozi wa Yemen.

Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah, mara nyingi alieleza furaha yake juu ya mafanikio ya wapiganaji wa Yemen, akitamani lau angekuwa miongoni mwao chini ya bendera ya kiongozi wao shujaa. Alijua kuwa watu wa Yemen ni alama ya muqawama – siyo kundi dogo la ndani, bali sehemu ya mhimili wa muqawama unaokabiliana na dhulma za Marekani na utawala wa Kizayuni.

Yemen katika Macho na Moyo wa Sayyid Hassan Nasrallah katika Miaka 11 ya Mapinduzi ya Yemen

Katika hotuba ya mwaka 2016, Sayyid Nasrallah alieleza vita dhidi ya Yemen kuwa ni “vita vya mauaji ya kimbari” na kuona jinai zilizotendwa humo kuwa ni kielelezo cha wazi cha mikakati ya kibeberu ya kuua utambulisho wa kitaifa wa Yemen. Mnamo 2018, katika kilele cha vita, alilitaja Yemen kama “uwanja mpya wa muqawama” dhidi ya dhulma ya kimataifa na uzayuni wa kikanda.

Aliposhuhudia ushindi wa Yemen kuonekana vitani, mwaka 2020 aliwapa bishara: “Wananchi wanaosimama imara na kusubiri mbele ya mitihani mikubwa hakika ndio watakaoibuka washindi.”

Na alipomsikia Sayyid Abdulmalik Houthi akisema: “Tuko tayari kugawana mkate wetu na Wapalestina,” huku machozi yakimtoka, Sayyid Hassan Nasrallah alisema: “Sayyid wangu, ninyi mko chini ya mzingiro, je, mna mkate wa kugawana? Wakati matajiri wengi wa Kiarabu na Kiislamu wana mabilioni ya dola katika mali zao binafsi...”

Kwa muda wote huu, Sayyid Hassan Nasrallah alisimama bega kwa bega na wananchi wa Yemen, akiwapa pole na pongezi wakati viongozi wao wakuu walipouawa, kama alivyomwandikia Abdulmalik al-Houthi baada ya kuuawa kwa Saleh al-Sammad, Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen.

Aidha, mara nyingi alilaani unyama wa muungano wa Saudi dhidi ya raia wa Yemen, hata masherehe na arusi, akisema: “Muungano wa wavamizi wa Saudi unawapiga hata furaha na tabasamu za watu wa Yemen.”

Yemen katika Macho na Moyo wa Sayyid Hassan Nasrallah katika Miaka 11 ya Mapinduzi ya Yemen

Katika kumbukumbu ya miaka 11 ya Mapinduzi ya Yemen, wananchi wa Yemen wanajiandaa kufanya maadhimisho ya kumbukumbu ya Sayyid mashahidi wa muqawama. Katika maandamano na mitandao ya kijamii, mara nyingi wametoa shukrani na heshima kwa Sayyid Hassan Nasrallah, ambaye kwa maneno na vitendo daima aliwapa moyo, akiwashirikisha uzoefu wa Hizbullah katika vita vya siku 33.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha